Saturday, November 6, 2010

mOurinho awapatanisha materazzi na zizou

HATIMAYE kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho
amezika tofauti kati ya Zinedine Zidane na Marco
Materazzi.
Wachezaji hao waligombana uwanjani katika
moja ya mechi za fainali ya Kombe la Dunia 2006
kati ya Italia na Ufaransa na kununiana kwa miaka
minne. Lakini wiki hii Mourinho amewapatanisha
na wachezaji hao walikumbatiana
.
Tukio hilo lilitokea katika hoteli ya kikosi cha Real
Madrid ambapo wachezaji wa Inter Milan walifika
kumsalimia kocha wao wa zamani.
Gazeti la Marca lisema: "Walimaliza ugomvi wao
na kuanza kuzungumza kama vile hawakuwa
mahasimu.

No comments:

Post a Comment